728x90 AdSpace

­
Latest News
July 17, 2014

SISTA APOTEZA MAISHA BAADA YA GARI ALILOKUWA AMEPANDA KUPINDUKA HUKO MTWARA.

Sista wa kanisa katoliki jimbo la Mtwara sista Sophia Nampwapwa amefariki dunia kwenye ajali mbaya ya barabarani, baada ya gari alilokisafiria kuacha njia na kupinduka mara 2 kwenye barabara ya chuno katika manispaa ya Mtwara/Mikindani.
Sista Sophia amefariki muda mfupi baada ya kufikishwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mtwara ya Ligula, na miongoni mwa viongozi waliostushwa na ajali hiyo na kufika hospitalini hapo kufuatilia, ni askofu wa jimbo la Mtwara Gabriel Mmole.
 
Kamanda wa polisi mkoa Mtwara kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Augustine Ollomi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo majira ya  saa 11 jioni, ikihusisha gari aina ya land rover lenye usajili namba T 589 AAG na kuongeza, polisi inamshikilia dreva wa gari hilo aliyetambulika kuwa Godwin, kwa uchunguzi zaidi.
 
Hata hivyo baadhi ya walioshuhudia ajali hiyo wamesema, imetokea wakati dreva alipokuwa akijaribu kumkwepa mpanda baskeli aliyekatisha ghafla barabarani huku dreva huyo akidaiwa, alikuwa kwenye mwendo kasi.
 
Akizungumzia kifo cha sista Sophia Nampwapwa kaimu mama mkuu shirika la masista wa mkombozi Mtwara sista Veronica amesema, wamepokea kwa mstuko mkubwa kifo hicho lakini wanawashukuru wote waliojaribu kuokoa maisha yake ikiwa ni pamoja waliombeba na kumwaisha hospitalini pamoja na madaktari.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 blogger-facebook:

Post a Comment

Item Reviewed: SISTA APOTEZA MAISHA BAADA YA GARI ALILOKUWA AMEPANDA KUPINDUKA HUKO MTWARA. Rating: 5 Reviewed By: Unknown