728x90 AdSpace

­
Latest News
July 17, 2014

MSUGUANO CHADEMA NA CCM:-TAZAMA PICHA WALIPOCHIMBANA MKWARA HUKU MKUTANO WA NAIBU WAZIRI WA MAJI UKIINGIA DOSARI KATIKA JIMBO LA UBUNGO..


Wafuasi wa Chama cha Mapinduzi CCM na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wakitaka kuzipiga kavu kavu baada ya kutokea mzozo ambapo wanaCCM walikuwa wakimzomea Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika  akihutubia na WanaChadema wakimzomea Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla  akihutubia katika mkutano huo Julai 15,2014.


Poilisi wakiwatuliza wafuasi wa CHADEMA waliokuwa wakipinga Mbunge wao John Mnyika asijibu swali lililoulizwa na Mkazi wa Kibamba, Jordan Balindo aliyemtaka Mnyika aeleze ni jitihada gani amezifanya binafsi kama mbunge kutatua changamoto ya ukosefu wa maji katika jimbo la Ubungo.



 Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Idd Azzan wa CCM (KULIA), akiamua ugomvi wa Diwani wa Kimara, Pascal Manota wa CHADEMA (kushoto) na Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge waliotaka kuzichapa baada ya kutokea mzozo katika mkutano wa hadhara wa Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla katika Uwanja wa Shule ya Mavurunza, Kata ya Salanga, Jimbo la Ubungo, Dar es Salaam jana(Julai 15,2014).


Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika (Chadema), wakitofautiana jukwaani wakati Makalla akiamuru polisi kuwatoa wafuasi wa Chadema waliokuwa wakimzomea wakati akileleza Utakelezaji wa Ilani ya CCM JUU YA MAJI, HUKU MNYIKA AKITAKA WAENDEE KUZOMEA AKIDAI KWAMBA WAZIRI HAKUFANYA HAKI KWANI YEYE ALIPOKUWA AKIZOMEWA NA WANA CCM HAKUWACHUKULIA HATUA KAMA HIYO KATIKA MKUTANO WA HADHARA ULIOFANYIKA KATIKA UWANJA WA SHULE YA MAVURUNZA, KATA YA SALANGA.

Jeshi la polisi limelazimika kumuokoa naibu waziri wa maji Mh Amosi Makala toka katikati mwa mikono ya makada wa Chadema na CCM katika kata ya Goba mara baada ya diwani wa viti maalumu CCM wa kata hiyo, alipokuwa akiwatambulisha makada wenzake wa CCM,kabla ya mkutano huo na wananchi kuvunjika kutokana na vurugu toka kwa makada wa Chadema na wale CCM.

Akiongea na waandishi wa habari akiwa ndani ya gari huku likiwa limezungukwa na ulinzi wa jeshi la polisi na makamanda wa CCM,naibu waziri wa maji amesema kuwa suala la maji halina itikadi na kuwa amesikitishwa na hatua hii ya kuwa nyima haki wananchi wengine kusikia sauti ya serikali kutokana an kero hiyo ya maji.

Wakiongea mara baada ya vurugu hizo mbunge wa jimbo la ubungo mh:john mnyika na mwenyekiti wa CCM wilya ya Kinondoni bwana Salumu Madenge kwa nyakati tofauti wameendelea kutupoiana vijembe huku kila mmoja akimalaumu kundi la mwenzake kuanzisha fujo.

Katika tukio lisilo kuwa la kawaida naibu waziri ameshuhudia matanki makubwa katika eneo la Kigogo nyumba mpya yanayo kadiriwa kuwa na ujazo lita laki moja na therahini,yakiwa yanatumika kuuzia maji kwenye magari ya maji hatua ambayo inadaiwa kuisababishia hasara ya mabilioni Dawasa na Dawasco.

Ziara hiyo ya naibu waziri wa maji iliyokuwa imeanzia maeneo ya Makongo juu,Mbezi na Goba maeneo ambayo yamekuwa hayana mfumo wa maji safi kabla ya ziara hiyi kukatishwa bila ya kuhutubia wananchi katika eneo la Goba,ambapo licha ya tukio hilo amesema kuwa kero ya maji itatatuliwa ifikapo September mwaka huu 2014.



Mfuasi wa CCM  akiwa na bango la kumshutumu Mbunge wa Jimbo hilo, John Mnyika.


Mfuasi wa Chadema akiwa na bango la kuishutumu Serikali.


 Polisi akilinda usalama mbele ya mashabiki wa CCM na CHADEMA.


Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Taka, Dar es Salaam, Eva Sinare (katikati) akijaribu kuunusuru mzozo huo kwa kuzungumza na Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika.


 Wafuasi wanawake wa CCM na Chadema wakichimbia mkwara.



Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akihutubia kwakueleza utekelezaji wa Ilani ya CCM, ambapo aliwahakikishia wananchi wa  jiji la Dares Salaam kwamba ifikapo mwishoni mwa mwaka ujao tatizo la maji litakuwa historia hasa baada ya kukamilika upanuzi wa Mtambo wa Maji wa Ruvu Juu ambao ujenzi wake umeanza sasa.


Wazir Makalla akipata maelezo kutoka kwa mkandarasi kuhusu ujenzi wa Tanki jipya la maji eneo la Kibamba, Dares Salaam,wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maji Dares Salaam na Pwani.


 Mkazi wa Kibamba, Chrisant Kibogoyo akiuliza swalikatika mkutanouliofanyika Kata ya Kibamba.


Mwalimu wa Shule ya Msingi ya Kibwegere, Hellen Mshana akiuliza swali kwa waziri kwambanilini maji yatasambazwa katika shule hiyo na zinginezo.


Askari akimuondoa mfuasi wa Chadema aliyekuwa akilazimisha kumuuliza swali Waziri Makalla katika mkutano huo.


Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Maji Safi na Taka Dares Salaam, (Dawasco), Jackson Midalla akijibu moja ya maswali yaliyoulizwa na Diwani wa Kata ya Kibamba, Issa Mtemvu wakati Waziri Makalla, alipotembelea mradi wa maji katika kata hiyo.


Wafuasi wa CCM  na Chadema wakishindana kupeperusha bendera za vyama vyao wakiwakwenye magari eneo la Kibamba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 blogger-facebook:

Post a Comment

Item Reviewed: MSUGUANO CHADEMA NA CCM:-TAZAMA PICHA WALIPOCHIMBANA MKWARA HUKU MKUTANO WA NAIBU WAZIRI WA MAJI UKIINGIA DOSARI KATIKA JIMBO LA UBUNGO.. Rating: 5 Reviewed By: Unknown