728x90 AdSpace

­
Latest News
July 17, 2014

MBUNGE WA TANZANIA ATUHUMIWA KUMPIGA BABA YAKE MZAZI

Moses Machali Kasulu Mjini
MBUNGE wa Jimbo la Kasulu mjini Moses Machali anatuhumiwa kumtwanga baba yake mzazi  Mzee Machali  sambamba na kumfukuza nyumbani kwake,kutokana na kitendo chake cha kulewa kupindukia ambayo imekuwa adha kwa mbunge huyo na kupelekea mgogoro mkubwa baina yake na mzazi  huyo.

Mbunge huyo amefikia hatua hiyo baada ya kuchoshwa na ulevi huo na kupelekea kumpa kichapo kilichosababisha kuteguka kwa mkono  sanjari na kumtupia nguo zake nje na hatimaye mzee huyo kukimbilia kwa Balozi wa nyumba kumi  Dickson Joaqim kwa msaada wa kisheria.

Awali Julai ,15, 2014 usiku mzee alichelewa kurudi nyumbani na alipomgongea mwanae afungue mlango ndipo akapata kichapo kutoka kwa mbunge huyo baada ya kuona adha hiyo ni sugu kwa mzee wake.
 
Akiongea kwa njia ya simu na mtandao huu mbunge huyo  alisema mzazi wake  anapenda kunywa pombe kupindukia hali inayomfanya kila wakati wagombane juu ya tabia hiyo ambapo kwa upande wa pili kisiasa inamuathiri katika uwajibikaji wake kwa wananchi.
Alisema baba yake anatumiwa na chama  cha ccm  kwa lengo la kumdhoofisha kisiasa hasa katika kipindi hiki cha majeruhi cha kuelekea uchaguzi mkuu mwakani na kumtaja balozi wa mtaa wa mwilavya  Dickson Joaqim ni miongoni mwa watu wanaomshawishi mzee wake  kituo cha polisi kumshtaki.

“sijafikia hatua ya kumpiga mzee wangu,najitambua ndio maana namsihi baba achane na pombe ambapo mimi najiskia vibaya kuona  analewa sasa tukiwekana sawa baadhi ya watu wanadai nampangia sheria na ndo hivyo wanazusha ya kuzusha” alibainisha Machali.
Alisema kwa  kuthibitisha  hilo umma kuwa hajampiga mzee wake  na kwenye mkutano wa hadhara wilayani hapo, atakuwa sambamba na mzee huyo na kukiri mzee wake amefuta kesi dhidi yake na kusisitiza ccm  watumie mbinu za ziada na kudai hawana jipya.
Shuhuda mmoja jina kapuni akiri kumuona  mzee huyo akiwa na `PF3′ akitembea kwa shida huku mkono wake ukiwa umevimba akipatiwa matibabu katika moja ya zahanati ya wilayani hapo
 
Akithibitisha  hilo Kamanda wa Polisi Mkoa Frasser Kashai alisema ni kweli mzee wake amefungua jalada la kumshataki mbunge huyo  na wao wanaendelea na uchunguzi zaidi ili kukamilisha taratibu za mashataka
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 blogger-facebook:

Post a Comment

Item Reviewed: MBUNGE WA TANZANIA ATUHUMIWA KUMPIGA BABA YAKE MZAZI Rating: 5 Reviewed By: Unknown