728x90 AdSpace

­
Latest News
July 12, 2014

PAPA FRANCIS Amteua Askofu Joseph Kulola Kuwa Askofu Mpya Jimbo la Kigoma.


Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis amemtua askofu Joseph Kulola kuwa askofu mpya wa Jimbo la Kigoma.
Akizungumza na Radio Kwizera kwa njia ya simu kutoka wilayani Biharamulo mkoani Kagera,inakoendelea awamu ya pili ya Sinodi kwa Jimbo Katoliki la Rulenge Ngara, Askofu Severine Niwemugizi wa Jimbo hilo amesema uteuzi huo umefanyika Julai 10,2014 majira ya mchana.

Amesema askofu huyo mteule ni mzaliwa wa Jimbo la Same, Mkoani Kilimanjaro ambaye kwa sasa ndiye mkuu wa Seminari ya Mt Paul iliyoko Kipalapala Mkoani Tabora.

Askofu mteule Kulola anayetokea Shirika la Kazi ya Roho Mtakatifu ameteuliwa kuchukua nafasi ya aliyekuwa askofu wa Jimbo la Kigoma askofu Protas Rugambwa ambaye kwa sasa yuko kwenye idara ya Uinjilishaji mjini Roma, Italia.


Habari Na:-Radio Kwizera FM-Ngara.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 blogger-facebook:

Post a Comment

Item Reviewed: PAPA FRANCIS Amteua Askofu Joseph Kulola Kuwa Askofu Mpya Jimbo la Kigoma. Rating: 5 Reviewed By: Unknown