Na katika nyayo za watangulizi wake, na hasa katika mwanga wa Paul VI , aliyefanya hija hii miaka hamsini iliyopita, na hivyo kuwa Papa wa kwanza kutembelea Nchi Takatifu ,pia alitamani sana kufanya hija hii ya kutembelea maeneo ambayo yamemshuhudia Yesu akiyaishi maisha haya ya kidunia. Na kwamba hija yake isingekuwa kamili bila ya kukutana na kutafakari pamoja na watu wanao ishi katika nchi hii. Na hivyo kwa heshima na taadhima ameweza kukutana na Mufti Mkuu wa Jerusalem , na Waislamu wengine , wake kwa waume.
Hotuba ya Papa ilielekeza mawazo kwa Ibrahimu , ambaye aliishi kama Mhujaji wa imani katika nchi hiI ambayo Waislamu, Wakristo na Wayahudi wanamtabua Ibrahimu kuwa Baba yao wa Imani, ingawa kila mmoja, humwabudu Mungu Mmoja katika njia tofaut. Ibarahim ni mfano mkubwa sana wa jinsi ya kumfuata Mungu kwa imani kuu.
Papa amewatia moyo waamini wote kwamba, katika Hija hii ya kidunia, hatuko peke yetu. Kwa Wakristo, kwa njia ya msalaba, huungana na waamini wa dini nyingine ,
kushiriki na kutembea pamoja na hata kuishi pamoja kama sehemu njia ya kutimiza mapenzi ya Mungu. Papa alitoa shukurani zake za dhati kwa wote walio wezesha mkutano huo na kwa ukarimu wao ulioonyesha kwamba , hija ya maisha, ni yetu sote binadamu . .
Papa aliomba uwepo wa mawasiliano ya kidugu na kubadilishana mawazo , kama hatua yenye kutoa mwanya wa chaguzi na nguvu mpya, katika kukabiliana na changamoto katika maisha ya kawaida, na wao kama viongozi waweze kuwa msitari wa mbele likabiliana na changamoto kwanza.
Alisema, hawawezi kusahau ,ukweli kwamba Hija ya Ibrahimu, pia ilikuwa ni wito kwa uadilifu : Mungu alimtaka aishuhudie imani yake kimatendo. Na hivyo , pia wao, kama viongozi, wangependa kuwa mashahidi wa utendaji wa Mungu katika dunia yetu. Aliomba kukutana kwao kutia shime vuguvugu la ndani la kusambaza wito huu na katika kuwa mawakala wa amani na haki” . Papa aliwasihi katika zawadi ya sala pia kujifunza kuwa na huruma kuu, kumheshimu kila mmoja na kupendana kama kaka na dada ! Pia kujifunza kuelewa maumivu mwingine !
Na jina la Mungu lisitumiwe kama chombo cha kuhalisha vurugu na maonevu, balijina hilo liwe kichocheo cha utendaji wa pamoja kwa ajili ya kujenga haki na amani!
Aidha Baba Mtakatifu , majira ya asubuhi, alikutana na Rabbi Wakuu wawili wa Israel, na pia alitembelea Makao makuu ya Rais wa Israel.
Baba Mtakatifu majira ya jioni kabla ya kuongoza Ibada ya Misa itakayokamilisha Hija yake katika nchi Takatifu , anakutana na Mapadre watawa na waseminaristi katika Kanisa la Getsemani.
0 blogger-facebook:
Post a Comment