Mtawa mmoja wa kanisa katoliki aliyefahamika kwa jina moja la sister
Kapuli ameuwawa kwa kupigwa risasi kichwani na watu wanaosadikiwa kuwa
ni majambazi katika eneo la River side Ubungo jijini Dar es Salaam na
kutoweka na pochi ya sister huyo inayodaiwa kuwa na fedha ambazo kiasi
chake hakikufahmika mara moja. Tukio hilo limetokea siku ya leo (23/06/2014) majira ya saa 7 na nusu mchana.
Risasi kama inavyoonekana eneo la tukio
Sr Kapuli wa parokea ya Makoka jijini Dar es Salaam
ameuwawa kwa kupigwa risasi kichwani na watu watatu wanaodaiwa kuwa ni
majambazi baada ya kufuatiliwa nyendo zao wakitokea katika benki ya CRDB
ambayo tawi lake halikufahamika mara moja wakati akimsubiri Sr Mwenzie
aliyeshuka katika gari walilokuwa wamepanda lenye namba za usajili T
213 CJZ Toyota VX kwa ajili ya kwenda kuulizia bidhaa fulani dukani
katika eneo hilo la Riverside Ubungo jijini Dar es Salaam.
Akisimulia tukio hilo dereva wa gari la masister
hao, Bwana Marck Patrick Mwarabu ameeleza kuwa majambazi hayo yalikuwa
matatu na alipojaribu kuyadhibiti kwa kufunga mlango wa gari walimjeruhi
vibaya kwa risasi katika dole gumba lake na kisha kutoweka na pochi ya
marehemu Kapuli kwa kutumia usafiri wa pikipiki.
kidole gumba cha dereva baada ya kupigwa risasi
Dereva baada ya kupigwa risasi katika kidole gumba
Mmoja wa waendesha bajaji bw Godfrey Severine
ambaye amenusurkakatika tukio hilo bada ya bajaji yake kupigwa risasi
kadhaa amesema kuwa watu hao walifyatua risasi kadhaa zilizosababisha
taharuki kwa wananchi ambao walikuwa wakikimbia hovyo na hivyo kupata
upenyo wa kutoweka katika eneo hilo.
Diwani wa kata ya Makuburi Bw William Mfungo
aliyeshuhudia pia tukio hilo amesema wakati umefikasasa kwa jeshi la
polisi kujizatiti kudhibiti matukio hayo kutokana na majambazi kutumia
silaha nzito ambazo wananchi hawawezi kupambana nao na kuwataka wananchi
kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi pale wanapobaini njama kabla ya
tukio kutokea.
Jeshi la polisi wakiwa na silaha walifika katika
eneo la tukio na kuondoka na mwili wa marehemi licha ya kukuta majambazi
hayo yameshatoweka katika eneo la tukio.
*bwana
ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe* Amen.
TANBIHI: Samahani kwa hizo picha hapo juu.
0 blogger-facebook:
Post a Comment