Wapendwa mwisho wa mwezi huu wa sita Baraza la maaskofu Katoliki Tanzania TEC litafanya mkutano wake mkuu wa mwaka kurasini Dar es salaam, Katika vipindi vya study
session wamechagua mada ya "VIJANA NA IMANI", Ungepata nafasi ya kushiriki je ungependa kuwaambia nini juu ya mada hii? Na je ungependa kuwauliza nini? , Na ungependa kuwashirikisha nini?
Kwa kuwa wote hatuwezi kupata nafasi ya kushiriki naomba kupitia jukwa hili walau tupate mawazo yenu juu ya mada hiyo ili yaweze kusaidia katika kuanda mada hiyo.
Yafatayo ni mwaswali yanayoweza kukusaidia katika kutoa mawazo yako.
1. Inasemekana vijana wengi tumekuwa wagumu wa kushiriki imani yetu hasa kusali, unadhani ni kwa nini? Je mtazamo huo ni sahii? Kama ni sahihi nini kifanyike?
2. Ni jambo gani katika imani yako katoliki linakuongezae imani? Naje ni lipi nilo kupunguzia imani? Kwa nini? Unashauri nini kifanyike?
3. Je mafundisho ya kanisa ni kikwazo katika maisha yako na furaha zako? Kama sio nini kinatufanya vijana tuchague maisha ya dhambi na sio amri za Mungu? Ugumu uko wapi?
4. Je ni fulsa zipi zilizopo ambazo unadhani kama kanisa litazitumia zitaweza kuongeza ushiriki mkubwa wa vijana katika kanisa?
5. Je upo karibu na kanisa? kama ni ndio kivipi? kama ni hapana ni kwa nini? Na ungependa nini kifanyike ili kuwavuta vijana zaidi na kanisa?
6. Je changamoto wanazokabiliana nazo leo vijana katika maisha ni zipi?
Zinachangia vipi katika kushuka kwa imani?
Hayo ni baadhi ya maswali lakini unaweza kutoa mawazo zaidi, jitaidi utume kabla ya jumatano tare 18 june, tuma kwa njia ya facebook,amail addres vifuko@costech.or.tz, ditrickruta78@yahoo.co.uk.
Mungu atubariki sote.
0 blogger-facebook:
Post a Comment