Sherehe ya Pentekoste ilifana kiaina katika Jimbo kuu la Dar es salaam ambapo Baba Askofu Eusebius Nzigilwa aliwapatia kipaimara vijana wapatao 214 katika parokia ya Damu Takatifu ya Yesu, Tegeta.
Vijana hao wamekuwa askari wa Yesu kwa kuimarishwa na mapaji saba ya roho Mtakatifu ambayo ni: Hekima, Akili, Shauri, Nguvu, Elimu, Ibada na Uchaji wa Mungu.
Tuzidi kuwaombea vijana hao ili waweze kuwa askari wazuri wa Yesu kwa kulitangaza neno lake.
"Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo,akimpendeza Mungu na wanadamu." Luka 2:52
Sherehe hiyo ya pentekoste iliyofanyika tarehe 08.06.2014 ilikuwa ya kipekee sana katika parokia nyingi jimbo kuu la Dar es salaam kutokana na uimbaji wa wanakwaya pamoja na watoto wa kipapa(utoto Mtakatifu) lakini pia upekee wa siku hiyo maana vyama vingi vya kitume vilijitolea sana katika kusherehesha siku hiyo muhimu.
0 blogger-facebook:
Post a Comment