WAAMINI wametakiwa kuwa makini juu ya maendeleo ya sayansi na teknolojia yanayoendelea duniani kote yasije yakawaondoa katika misingi wa imani waliyonayo ndani ya Kanisa.
Hayo yamezungumzwa na Askofu Ludovick Minde wa Jimbo Katoliki Kahama alipokuwa akifunga mwezi wa Rozali Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Karoli Lwanga parokia ya Kahama mjini.
“ Wakristo sasa hivi katika maisha yetu tumezingirwa na mambo mengi katika dunia hii ya sayansi na teknolojia mnapaswa kuwa waagalifu na kusimama imara katika mafundisho na mapokeo ya Kanisa,” Amesema Askofu Minde.
Askofu Minde aliwataka waumini kukufua moyo wa sala kwa Mama Bikra Maria kwa kila muumini , familia , jumuiya na kwa Kanisa lote katika shida mbalimbali wataweza kushuhudia makuu kwenye maisha yetu ya kila siku.
Alisema sala ya Rozali Takatifu ni alama ya kumshukuru Mungu kwa zawadi ya Mama Bikra Maria anayetujali fadhili nyingi binafsi katika mioyoni mwetu , amani familia, jumuiya, taifa letu na kwa kanisa kwa ujumla.
0 blogger-facebook:
Post a Comment