728x90 AdSpace

­
Latest News
June 23, 2014

MTAWA AUWAWA KWA KUPIGWA RISASI NA MAJAMBAZI JIJINI DAR ES SALAAM


Mtawa mmoja wa kanisa katoliki aliyefahamika kwa jina moja la sister Kapuli ameuwawa kwa kupigwa risasi kichwani na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi katika eneo la River side Ubungo jijini Dar es Salaam na kutoweka na pochi ya sister huyo  inayodaiwa kuwa na fedha ambazo kiasi chake hakikufahmika mara moja. Tukio hilo limetokea siku ya leo (23/06/2014) majira ya saa 7 na nusu mchana.

 Risasi kama inavyoonekana eneo la tukio

Sr Kapuli wa parokea ya Makoka jijini Dar es Salaam ameuwawa kwa kupigwa risasi kichwani na watu watatu wanaodaiwa kuwa ni majambazi baada ya kufuatiliwa nyendo zao wakitokea katika benki ya CRDB ambayo tawi lake halikufahamika mara moja wakati akimsubiri Sr Mwenzie aliyeshuka katika gari walilokuwa wamepanda lenye namba za usajili  T 213 CJZ  Toyota VX kwa ajili ya kwenda kuulizia bidhaa fulani dukani katika eneo hilo la Riverside Ubungo jijini Dar es Salaam.

Akisimulia tukio hilo dereva wa gari la masister hao, Bwana Marck Patrick Mwarabu ameeleza  kuwa majambazi hayo yalikuwa matatu na alipojaribu kuyadhibiti kwa kufunga mlango wa gari walimjeruhi vibaya kwa risasi katika dole gumba lake na kisha kutoweka na pochi ya marehemu Kapuli kwa kutumia usafiri wa pikipiki.

 kidole gumba cha dereva baada ya kupigwa risasi

 Dereva baada ya kupigwa risasi katika kidole gumba

Mmoja wa waendesha bajaji bw Godfrey Severine ambaye amenusurkakatika tukio hilo bada ya bajaji yake kupigwa risasi kadhaa amesema kuwa watu hao walifyatua risasi kadhaa zilizosababisha taharuki kwa wananchi ambao walikuwa wakikimbia hovyo na hivyo kupata upenyo wa kutoweka katika eneo hilo.

Diwani wa kata ya Makuburi Bw William Mfungo aliyeshuhudia pia tukio hilo amesema wakati umefikasasa kwa jeshi la polisi kujizatiti kudhibiti matukio hayo kutokana na majambazi kutumia silaha nzito ambazo wananchi hawawezi kupambana nao na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi pale wanapobaini njama kabla ya tukio kutokea.

Jeshi la polisi wakiwa na silaha walifika katika eneo la tukio na kuondoka na mwili wa marehemi licha ya kukuta majambazi hayo yameshatoweka katika eneo la tukio.
*bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe* Amen.
TANBIHI: Samahani kwa hizo picha hapo juu. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 blogger-facebook:

Post a Comment

Item Reviewed: MTAWA AUWAWA KWA KUPIGWA RISASI NA MAJAMBAZI JIJINI DAR ES SALAAM Rating: 5 Reviewed By: Unknown